Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 31 YA 31

Waliokuwa wanatoza ushuru wa nusu shekeli ni viongozi wa hekalu la Mungu Yerusalemu. Thamani ya nusu shekeli ni sawa na malipo ya kazi ya kibarua ya siku mbili Tanzania. Kwa mfano huu Yesu anataka kusema kwamba yeye na wanafunzi wako huru, wasingehitaji kulipa, maana Yesu ni mwana wa Mfalme wa Mbinguni na wanafunzi wake ni watoto wa Mungu. Wao si wageni. Yesu ameleta majira mapya. Shughuli za hekalu zinaelekea kwisha. Kwa siku zijazo hekalu la Mungu litakuwa ni mioyo ya watu wanaomwamini Yesu.

siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz