Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 27 YA 31

Kazi yachachuinafanana na kazi ya hamira. Chachu kidogo tu ikiwekwa ndani ya unga uliokandwa itaenea katika unga wote na kuumua. Lakini chachu pia ni tofauti na hamira, maana chachu ina harufu ya uchungu ambayo inaibadilisha harufu yote ya unga wote. Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi Mafarisayo hawakumtambua. Hii inaonyesha kwamba hawakuongozwa na Roho wa Mungu. Mafundisho yao ni kama chachu mbaya, kwa hiyo wanafunzi wa Yesu wajilinde na mafundisho hayo! Nasi tujilinde! Fanya hivyo kwa kuzingatia m.11-12:Imekuwaje hamkufahamu ya kuwa si kwa sababu ya mkate naliwaambia? Ila jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.Ndipo walipofahamu ya kuwa hakuwaambia kujilinda na chachu ya mkate, bali na mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz