Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 25 YA 31

Yesuhakumjibu neno(m.23). Huenda wewe pia uliwahi kuona hivyo ulipomwomba Yesu akusaidie katika jambo fulani. Huenda hata wewe unauguliwa na mtoto. Lakini Yesu amenyamaza tu. Ni kama hasikii. Hupati nafuu. Basi, neno la leo likusaidie. Kwanza utambue kwamba sisi wanadamu hatustahili lolote kwa Mungu, maana ni wenye dhambi na tunaishi katika ulimwengu wa dhambi. Hatuwezi kudai, ila kuomba tunaweza, tukiitegemea neema yake. Somo linatutia moyo tusichoke kuomba bali tudumu katika maombi:Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa; kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa. Au kuna mtu yupi kwenu, ambaye, mwanawe akimwomba mkate, atampa jiwe? Au akiomba samaki, atampa nyoka? Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?(Mt 7:7-11).

siku 24siku 26

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz