Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 24 YA 31

Yesu anafundisha juu ya usafi wa kiroho. Katika hili Mafarisayo na waandishi walikwenda kinyume cha ukweli wa Mungu kwa njia mbili:1.Waliyahesabumafafanuziya sheria (mapokeo yao; m.3) kuwa muhimu kuliko sheria zenyewe za Mungu:Mbona ninyi nanyi huihalifu amri ya Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu? Kwa kuwa Mungu alisema, Mheshimu baba yako na mama yako, na Amtukanaye baba yake au mama yake kufa na afe. Bali ninyi husema, Atakayemwambia babaye au mamaye, Cho chote kikupasacho kusaidiwa na mimi ni wakfu, basi asimheshimu baba yake au mama yake. Mkalitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu!(m.3-6) Tulipokee fundisho la Yesu. Tusiwe tunahesabu mafafanuzi yetu ya neno la Mungu (theolojia yetu) kuwa sawa na, au hata juu ya neno la Mungu!2.Walikuwa wanaangalia usafi wa nje tu. Lakini hautoshi kwa Mungu. Zingatia maana ya maneno yafuatayo kwako:Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami(m.8). Vituvitokavyo kinywani vyatoka moyoni; navyo ndivyo vimtiavyo mtu unajisi.Kwa maana moyoni hutoka mawazo mabaya, uuaji, uzinzi, uasherati; wivi, ushuhuda wa uongo, na matukano;hayo ndiyo yamtiayo mtu unajisi; lakini kula kabla hajanawa mikono hakumtii mtu unajisi(m.18-20).

siku 23siku 25

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz