Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 23 YA 31

Yesu alitembea juu ya maji. Hata Ulaya watu hutembea juu ya maji. Lakini watu hawalihesabu kama mwujiza, maana wakati wa baridi maji yanaganda na kugeuka kuwa magumu. Ikiwa ni baridi sana hata magari huweza kupita juu yake! Ila katika nchi za joto kama Tanzania au Israeli maji hayagandi, na mtu hawezi kutembea juu yake bila kuzama. Kwa Yesu iliwezekana kwa sababu ni Mwana wa Mungu. Ndivyowaliokuwa ndani ya chombowalivyoona na kuamini walipomwona Yesu kutembea juu ya maji,wakamsujudia, wakisema, Hakika wewe u Mwana wa Mungu(m.33).Vyotevilifanyika kwa huyo(hata maji!); wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika(Yn 1:3).

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz