Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

SIKU 22 YA 31

Yesu aliposikia hayo, aliondoka huko katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, faraghani(m.13). Yesu alikuwa amesikia nini? Katika m.1-2 imeandikwa:Wakati ule mfalme Herode alisikia habari za Yesu, akawaambia watumishi wake, Huyo ndiye Yohana Mbatizaji; amefufuka katika wafu; na kwa hiyo nguvu hizo zinatenda kazi ndani yake. Maneno haya yaliwafanya Mafarisayo kumwonya Yesu:Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua(Lk 13:31). Maisha ya Yesu yalikuwa hatarini, lakini wakati wake ulikuwa bado haujatimia. Kwa hiyo aliepukana na hiyo hatari kwa kufanya mambo mawili:1.Alitumia akili yake:Aliondoka huko. Aliamua kwendaBethsaida, yaani kwenye eneo la mfalme mwingine aliyeitwa Filipo.2.Alimkimbilia Baba yake kwa sala:Akaenda ... faraghani(Lk 9:10). Katika kufanya mambo hayo ni mfano kwetu.

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku 07/2024

Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz