Soma Biblia Kila Siku 07/2024Mfano
Msimwambie mtu ye yote habari ya maono hayo, hata Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu(m.9). Agizo hili alitoa Yesu ili watu wasije wakamfanya kuwa mfalme. Katika Yn 6:14-15 tunasoma kwamba ndivyo wengine walivyotaka kufanya, hata kwa kutumia nguvu:Watu wale walipoiona ishara aliyoifanya, walisema, Hakika huyu[Yesu]ni nabii yule ajaye ulimwenguni. Kisha Yesu, hali akitambua ya kuwa walitaka kuja kumshika ili wamfanye mfalme, akajitenga, akaenda tena mlimani yeye peke yake(Yn 6:14-15).Na mtume Petro kweli alieleza habari hii, kwa sababu baada ya ufufuo aliandika wazi juu ya hilo aliloliona akiwa mlimani pamoja na Yesu:Hatukufuata hadithi zilizotungwa kwa werevu, tulipowajulisha ninyi nguvu zake Bwana wetu Yesu Kristo na kuja kwake; bali tulikuwa tumeuona wenyewe ukuu wake.Maana alipata kwa Mungu Baba heshima na utukufu, hapo alipoletewa sauti iliyotoka katika utukufu mkuu, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.Na sauti hiyo sisi tuliisikia ikitoka mbinguni tulipokuwa pamoja naye katika mlima ule mtakatifu(m.16-18). Katika mistari inayofuata (m.19-21) Petro anatukumbusha matokeo fulani ya tukio hilo:Tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ing'aayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya asubuhi kuzuka mioyoni mwenu.Mkijua neno hili kwanza, ya kwamba hakuna unabii katika maandiko upatao kufasiriwa kama apendavyo mtu fulani tu.Maana unabii haukuletwa po pote kwa mapenzi ya mwanadamu; bali wanadamu walinena yaliyotoka kwa Mungu, wakiongozwa na Roho Mtakatifu.Yesu kuonekana katika utukufu pamoja na manabii wawili wakuu kwenye mlima, kulithibitisha kwa Mtume Petro kwamba neno la manabii ni kweli kabisa. Kwa hiyo anatuhimiza kwamba tuliangalie neno laokama taa ing'aayo mahali penye giza.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku 07/2024 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa saba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Waebrania na Mathayo. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz