Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Palikuwa na manung’uniko(m.1). Tusishangae yakitokea manung’uniko hata kwetu siku hizi, maana ndivyo ilivyokuwa katika kanisa la kwanza! Lakini pia tuzingatie namna walivyoyatatua!1.Walikubali kwamba shida ipo. Hawakubisha.2.Wakashauriana.3.Wakajulisha uamuzi wao kwa wote na kutoa maelezo.4.Baada ya uamuzi wao kukubalika na mkutano wakautekeleza.5.Wakamkabidhi Mungu jambo hili kwa kuomba, kama ilivyandikwa katika Mit 16:3,Mkabidhi Bwana kazi zako, na mawazo yako yatathibitika. Katika m.3-4 imeandikwa,Basi ndugu, chagueni watu saba miongoni mwenu, walioshuhudiwa kuwa wema, wenye kujawa na Roho, na hekima, ili tuwaweke juu ya jambo hili;na sisi tutadumu katika kuomba na kulihudumia lile Neno. Tafakari maana ya neno hili. Ukipenda, linganisha na Kut 18:13-26!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/