Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kuna watu mpaka leo hasa katika maeneo ya Mission tunapoenda kufanya uinjilisti tunawakuta; wengi wakubwa na watoto wamevaa hirizi shingoni na kiunoni, tulipowauliza wakasema ni kwa ajili ya ulinzi dhidi ya wachawi na magonjwa, hivyo wanalala kwa furaha wanadhani wapo salama. Mwimba zaburi hii anasema “amtumainiye Bwana fadhili zitamzunguka”(m.10b). Mtu wa Mungu anafuraha siku zote kwa sababu anamtegemea Bwana Yesu na sio hirizi. Ameshagaramia ulinzi mtegemee yeye kwa furaha. Amen.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/