Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Tukipitishwa kwenye majaribu hadi kuyashinda, jambo hilo hutuimarisha katika imani yetu kwa Mungu. Tena hutupa ujasiri wa kumshuhudia Mungu wetu kwa yale matendo makuu ambayo anatutendea. Mwandishi anakumbuka jinsi Mungu alivyomwokoa wakati uliopita:Amenitendea fadhili za ajabu katika mji wenye boma. Nami nalisema kwa haraka yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya dua yangu wakati nilipokulilia(m.21-22). Kwa matokeo hayo ya matendo ya Mungu, anahamasisha watu wote wampende Mungu na kumtumaini kwa uvumilivu na ujasiri. Kushinda majaribu kwa njia hiyo kunatupa uzima, ujasiri na nguvu za kumshuhudia Mungu maishani.Heri mtu astahimiliye majaribu; kwa sababu akiisha kukubaliwa ataipokea taji ya zima, Bwana alivyowaahidia wampendao(Yak 1:12).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/