Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kuna mtu mmoja aliwahi kushuhudia jinsi alivyokosa furaha katika maisha yake. Alisema alivunja mmoja ya amri kumi za Mungu kwa siri, halafu akawa anajaribu kusahau lakini alishindwa kwani hata akilala alipata shida sana, Roho wa Mungu iliendelea kumwonyesha kosa lake. Siku moja akaamua kwenda kutubu. Tangu siku ile alipata furaha kubwa moyoni mwake na kusahau dhambi yake. Angalia maisha yako kama huna furaha, nawe ukatubu. “Heri aliyesamehewa dhambi na kusitiriwa makosa yake”(m.1).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/