Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Unapopatwa na shida au ukiwa na uhitaji, je, ni nani aliye msaada wako? Mwanadamu ameumbwa katika hali ya kumtegemea Muumba wake. Ingawa mategemeo mengine huwa hayana msaada wala maana yoyote, inatokea mara nyingi tunayakimbilia. Daudi amemchagua BWANA kuwa mchungaji wake, na anatolea ushuhuda jinsi ambavyo BWANA amemsaidia katika mengi wakati wa dhiki zake. Zaburi hii ilimsaidia hata Yesu akiwa msalabani (ling. m.5 na Lk 23:46,Mikononi mwako naiweka roho yangu; umenikomboa, Ee Bwana, Mungu wa kweli ...Yesu akalia kwa sauti kuu, akasema, ee Baba, mikononi mwako naiweka roho yangu). BWANA ndiye kimbilio lililo sahihi kwa kila mmoja wetu. Tumtegemee!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/