Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Ni nini siri ya Mwimba Zaburi kuwa na ujasiri mkuu hivi, hata kumwalika Mungu amhukumu, ampime na kumjaribu? Jibu lipo kuanzia m.1: Anakwenda kwa ukamilifu wake (m.1b). Ndiyo sawa na mtu anayekwenda bila hila katika kweli ya Mungu, akimtumaini Bwana bila wasiwasi (m.1c). Daima anakazia macho yake kwa fadhili zake Mungu na masikio yake kwa neno la kweli la Mungu (m.1c na 3). Angalia kwamba hayo yote anafanya kwa kutegemea si yeye mwenyewe bali utakaso wa Mungu (m.2b). Utakaso huo unafanyika Mwimba Zaburi anapojiepusha na uovu kwa kukaa nyumbani mwa Mungu:Nimelichukia kusanyiko la watenda mabaya, wala sitaketi pamoja na watu waovu ... Bwana, nimependa makao ya nyumba yako(m.5-8). Je, wewe unao ujasiri kama huo? Umtafute kwanza Bwana aliye tayari kukutakasa katika Kristo Yesu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/