Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Stefano aliposimulia habari ya Musa, pia alifafanua kidogo maana yake. Musa alikuwa na elimu kubwa sana na alijulikana kama mwana wa Farao (m.21-22,Hata [Musa] alipotupwa, binti Farao akamtwaa, akamlea awe kama mwanawe.Musa akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa hodari wa maneno na matendo).Akataka kuwasaidia watu wake Waisraeli akitegemea uwezo wake.Alidhani kwamba ndugu zake watafahamu ya kuwa Mungu anawapa wokovukwa mkono wake, lakini hawakufahamu(m.25). Hapa twajifunza kwamba kazi ya Bwana tusiifanye kwa kutegemea uwezo wetu. Tukifanya hivi nasi tutashindwa. Lazima Bwana mwenyewe atutangulie (m.35-36,Musa huyo waliyemkataa, wakisema, Ni nani aliyekuweka kuwa mkuu na mwamuzi? Ndiye aliyetumwa na Mungu kuwa mkuu na mkombozi, kwa mkono wa yule malaika aliyemtokea katika kile kijiti.Huyo ndiye aliyewatoa, akifanya ajabu na ishara katika nchi ya Misri, na katika bahari ya Shamu, na katika jangwa muda wa miaka arobaini)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/