Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023

SIKU 6 YA 32

Myahudi Stefano aliwaeleza Wayahudi wenzake juu ya historia yao. Aliwakumbusha kwamba Musa na manabii wengine walitabiri juu ya Yesu Kristo (kuhusu Musa imeandikwa katika m.37,Musa huyo ndiye aliyewaambia Waisraeli, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye. Na katika m.52 Stefano anajumlisha manabii wengine wote akisema,Ni yupi katika manabii ambaye baba zenu hawakumwudhi? Nao waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki). Lakini hapo zamani Wayahudi walimwasi Musa na kuwaudhi manabii (m.39,Mtu huyo [Musa] baba zetu hawakutaka kumtii, bali wakamsukumia mbali). Na roho ile ya kumpinga Roho Mtakatifu ndiyo hao Wayahudi wa sasa wanayoiendeleza! Wana shingo ngumu!Waliwaua wale waliotabiri habari za kuja kwake yule Mwenye Haki; ambayeninyi sasa mmekuwa wasaliti wake, mkamwua(m.52). Je, moyoni wako una hali gani?

siku 5siku 7

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/