Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023

SIKU 9 YA 32

Mchawi Simoni alikuwa amewashangaza watu wote kwa uchawi wake, hata waliomsikiliza waseme,Mtu huyu ni uweza wa Mungu, ule Mkuu(m.10). Lakini akaokoka kwa mahubiri ya Filipo, naakashangaa alipoziona ishara na miujiza mikubwa inayotendekakatika jina la Yesu Kristo (m.12-13)! Alikutana na uwezo ulio mkuu kuliko uwezo wa Shetani! Hata hivyo akajaribiwa. Akataka aonekane tena mbele ya watu kama mtu mkubwa akitumia nguvu ya Mungu.Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu(m.18-19). Akakemewa iliasinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani(Rum 12:3). Karama za Mungu zatolewa kwa neema naRoho huyo mmoja, yeye yule, akimgawia kila mtu peke yake kama apendavyo yeye(1 Kor 12:11)!

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/