Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Badala ya kuwakamata Wakristo wa Dameski, Sauli akawa anaitetea Injili kwa nguvu! Huu ni mwujiza wa Bwana! Huenda ulikuwa ni jibu la maombi ya Wakristo wa Dameski! Maana Yesu aliwaagiza wanafunzi wake:Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako; lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi(Mt 5:43-44). Stefano alifanya hivyo. Aliwaombea wauaji wake,Bwana, usiwahesabie dhambi hii(7:60). Na Sauli alikuwa mmojawao!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/