Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kornelio hakuwa Myahudi, ila alipewa sifa ya kuwamchaji wa Mungu(m.2 na 22). Yaani alikuwa ameipokea imani ya Wayahudi bila kujiunga kabisa na Uyahudi akitahiriwa na kuzitii amri zote za sheria ya Musa. Sheria ya Musa ilitoa k.m. amri juu ya wanyama walio safi na wasio safi. Kwa hiyo Bwana alipomwagiza Petro katika maono kwamba ale nyama isiyo safi (m.11-16), alikuwa na maana kwamba wokovu katika Yesu Kristo pia ni kwa wasio Wayahudi. Katika Kristo kuna umoja! Ukitaka kuchunguza zaidi jambo hili, unaweza kujisomea Efe 2:11-18.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/