Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kanisa jipya Antiokia lilipatamsaada wa kirohokutoka kanisa mama Yerusalemu. Wakamtuma Barnaba ili awaimarishe (m.22-23,Habari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwako katika Yerusalemu; wakamtuma Barnaba, aende hata Antiokia.Naye, alipokwisha kufika na kuiona neema ya Mungu akafurahi, akawasihi wote waambatane na Bwana kwa kusudi la moyo). Alipoona kazi imezidi sana, akamtafuta Sauli ili amsaidie.Ikawa kwa muda wa mwaka mzima wakakusanyika pamoja na kanisa na kuwafundisha watu wengi. Na wanafunzi waliitwa Wakristo kwanza hapo Antiokia(m.24-26). Pia walisaidiwa na manabii kutoka Yerusalemu (m.27,Siku zizo hizo manabii walitelemka kutoka Yerusalemu hata Antiokia). Wakristo wa Antiokia walikuwa wenye mali kuliko Wakristo wa Yerusalemu na Uyahudi. Kwa hiyo njaa kubwa ilipotokea duniani wakatumamsaada wa kimwilikwa ndugu zao. Je, sisi Wakristo wa Tanzania leo tunasaidiana kimwili na kiroho kama hao?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/