Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kanisa la Yerusalemu lilipata tena taabu. Mtume Yakobo aliuawa na mtume Petro alifungwa gerezani. Katika taabu yao walifanya nini?Kanisa likamwomba Mungukwa juhudikwa ajili yake(m.5),nawatu wengiwalikuwa wamekutana humo wakiomba(m.12). Walijibiwa kwa sababu ya imani kubwa? Hapana. Maana Roda alipowaambia kwamba Petro yupo mlangoni hawakumwamini (m.13-15)! Walijibiwa kwa maana waliombawengikwabidiikwajina la Yesu! Jifunze zaidi kwa kusoma Yn 14:13-14 na Lk 18:1-8.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/