Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Suala la waumini wa kimataifa kuhesabiwa kuwa Wakristo kamili bila kufuata sheria zote za Kiyahudi (k.m. kutahiriwa) lilileta mashaka katika kanisa la Yerusalemu. Kwa hiyo walishindana na Petro wakisema,Uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao(m.1-4). Hapo waumini wote walikuwa ni Wakristo wa Kiyahudi. Lakini baada ya Petro kutoa maelezo wakatulia na kumsifu Mungu. Katika m.17-18 imeandikwa kwamba Petro aliwauliza,Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu? Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba liletalo uzima. Roho Mtakatifu na ubatizo hufungamana. Ndivyo Petro alivyothibitisha siku ya Pentekoste,Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu(2:38). Huko kwa Kornelio, Roho aliwashukia kabla, basi Petro aliagiza wabatizwe. Ilikuwa ni kamaPentekoste kwa mataifa(kwa kulitafakari jambo hili zaidi, linganisha m.15-17 na Mdo 2:1-4).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/