Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Miujiza mikubwa ilifanyika kwa kupitia mtume Petro. Ishara hizi zilithibitisha ukweli wa neno la Injili lililohubiriwa na waumini katika miji hii. Kwa hiyo ikawafanya watu wengi sana wamgeukie Bwana:Watu wote waliokaa Lida na Sharoni wakamwona, wakamgeukia Bwana(m.35).Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana(m.42). Kumfufua mfu ni mwujiza wa pekee sana uliotukia mara chache tu. Yesu mwenyewe alifanya hivyo mara chache, akasema:Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya (Yn 14:12). Wakristo fulani hupewa karama ya kutenda miujiza (1 Kor 12:10,Kwa Roho apewa ... mwingine matendo ya miujiza).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/