Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Sauli akaliharibu kanisa(m.3). Baadaye alijulikana kama mtume Paulo. Lakini kwa wakati huu huonekana kama kiongozi wa ile adha kuu ya kanisa iliyoanza Yerusalemu siku alipouawa Stefano. Ingawa ni kijana tu, Sauli alikuwa ni mtu maarufu. Ikiandikwa katika m.58 kwambamashahidi wakaweka nguo zao miguuni pa kijana mmoja aliyeitwa Sauli,maana yake ni kwamba alisimamia tendo la kumwua Stefano. Yesu alikuwa amewaagiza wanafunzi wake wawe mashahidi wake pia katika Uyahudi wote, na Samaria (1:8,Mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi). Lakini mpaka sasa walikuwa wamebaki Yerusalemu tu! Ila hiyo adha kuu ikasababisha Injili ienee pia sehemu nyingine. Katika m.1 zimetajwaUyahudi na Samaria. Zingatia Wakristo walifanya ingawa walipatwa na adha kuu:Wale waliotawanyika wakaenda huko na huko wakilihubiri neno(m.4).Filipo alizihubiri habari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake(m.12)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/