Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kushini nchi ya Ethiopia. Kwa hiyo somo hili latueleza jinsi Injili ilivyofika bara la Afrika mara ya kwanza!Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu(m.35). Jambo kuu kwa kanisa la kwanza lilikuwa ni kusoma, kuhubiri na kushuhudianeno la Bwanaili watu wamjue Yesu (ukiwa na nafasi, rudia m.4-6, 12 na 25)! Je, hili pia ni jambo la msingi kwa kanisa la Tanzania leo? Je, wanaomtafuta Mungu wanafundishwa neno la Bwana ili waimarike? Tafakari swali hili ukikumbuka yule towashi alivyosema na kufanya:Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye(m.31)?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/