Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023

SIKU 12 YA 32

Anania akaenda ... akamwekea mikono akisema, Ndugu Sauli, Bwana amenituma(m.17). Yesu alisema na mwanafunzi wake Anania katika maono kwamba aende akamsaidie Sauli. Kwanza Anania hakupenda. Aliogopa. Lakini baada ya kuelezwa na Bwana juu ya mpango wake kuhusu Sauli akakubali kwenda:Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu(m.15-16). Labda wakati fulani Bwana pia husema na wewe rohoni mwako. Huenda anataka umwombee au umwendee mtu fulani ili umsaidie kiroho au kimwili. Basi uwe mtiifu, usikawie! Zingatia Yak 5:19-20,Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;
20 jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.

siku 11siku 13

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/