Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Stefano aliwaambia wazee wa baraza ukweli bila kuficha na bila hofu. Waliposikia maneno yake wakachomwa mioyo yao, lakini badala ya kutubu wakawa na hasira kubwa juu yake (hatawakamsagia meno;m.54). Kuna matukio mawili yanayotuonyesha kwamba Stefano kweli alijaa Roho Mtakatifu.1.Aliona mbingu zimefunguka (m.55-56,Yeye akijaa Roho Mtakatifu, akakaza macho yake, akitazama mbinguni, akauona utukufu wa Mungu, na Yesu akisimama upande wa mkono wa kuume wa Mungu.Akasema, Tazama! Naona mbingu zimefunguka, na Mwana wa Adamu amesimama mkono wa kuume wa Mungu.).2.Akawaombea wale waliomwua:Bwana, usiwahesabie dhambi hii(m.60). Ndivyo Yesu mwenyewe alivyoomba msalabani:Baba, uwasamehe, kwa kuwa hawajui watendalo(Lk 23:34). Na ametufundisha sisi kufanya vilevile:Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi(Mt 5:44). Je, unamwombea adui yako?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/