Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Kuhani Mkuu na watu wake walishindwa kuwakomesha mitume kwa sababu walipendwa na kuheshimiwa na umati mkubwa wa watu. Hatajamii kubwa ya makuhani wakaitii ile Imani(6:7). Kwa hiyo wakajaribu kuliharibu kanisa kwa kumkomesha Mkristo maarufu ambaye si mtume yaani Stefano. Lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye(6:10). Basi ikabidi watumie hila na ujanja ili kumkamata na kumshitaki (6:11-15,Hata wakashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.Wakawataharakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza.Wakasimamisha mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati;maana tumemsikia akisema kwamba Yesu huyo Mnazareti atapaharibu mahali hapa, na kuzibadili desturi tulizopewa na Musa.Watu wote walioketi katika ile baraza wakamkazia macho yao, wakamwona uso wake kuwa kama uso wa malaika). Stefano akaanza kujitetea kwa kusimulia historia yao.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/