Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Leo ni Jumapili ya kwanza ya Majilio. Bwana Yesu anaeleza kuhusu huduma yake hapa duniani. Ametumwa na Mungu kuleta habari njema kwa maskini, wagonjwa na wafungwa, wote wawekwe huru. Habari hizi hazikupokelewa vema kwa watu wa Nazarethi alipoishi. Walijifanya kumfahamu na kumzoea, na hivyo hawakuona wana haja ya kumpokea na kuwa naye kama mkombozi. Hata wakataka kumwua. Hii inatuonyesha ni hatari kuishi na Yesu kwa mazoea bila kumpokea akae ndani yetu. Tuombe Roho wa Mungu afungue macho na mioyo yetu ili tumpokee Yesu kweli kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/