Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023Mfano
Somo hili laweza kutusaidia hata leo Tanzania. Stefano alipewa kazi ya diakonia pamoja na wengine sita (m.1-2 na 5-6). Hata siku hizi ni muhimu viongozi wa kanisa wagawane majukumu, ili karama za Wakristo zifanye kazi kwa faida ya wote:Kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu(1 Pet 4:10)! Kwa kupewa wajibu Stefano akakua kiroho. Ikaonekana Mungu anataka kumtumia kwa kazi kama ile ya mitume ingawa si mtume (m.8-10,Na Stefano, akijaa neema na uwezo, alikuwa akifanya maajabu na ishara kubwa katika watu.Lakini baadhi ya watu wa sinagogi lililoitwa sinagogi la Mahuru, na la Wakirene, na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka na kujadiliana na Stefano;lakini hawakuweza kushindana na hiyo hekima na huyo Roho aliyesema naye). Huenda inatokea hata Tanzania kuwa Mungu humpa Mkristo uwezo wa kufanya kazi ya uchungaji ingawa si mchungaji!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Desemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Desemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Matendo ya Mitume. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/