Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 1 YA 29

Sehemu kuu ya kwanza ilihusuimaniya Mkristo. Leo tunaanza na sehemu kuu ya pili kuhusumatendoya Mkristo. Ndiyo ibada yenu yenye maana(m.1). Wakristo wengi Tanzania wanashiriki sana katika ibada ya Jumapili. Hili ni jambo zuri na linakusaidiakufanywa upya nia yako, upate kujua hakika mapenzi ya Mungu(m.2). Lakini usiwe Mkristo wa Jumapili tu. Ibada yenye maana inayompendeza Yesu ni kujikabidhi mikononi mwake kila siku na kumtumikia kwa hali na mali.Toeni miili yenu(m.1). Tafakari pia 6:13,Msiendelee kuvitoa viungo vyenu kuwa silaha za dhuluma kwa dhambi; bali jitoeni wenyewe kwa Mungu kama walio hai baada ya kufa, na viungo vyenu kwa Mungu kuwa silaha za haki.

siku 2

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/