Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 7 YA 29

Somo linahusu vitendo ambavyo kwa Mkristo mmoja ni dhambi na kwa mwingine si dhambi. Neno la Mungu halisemi vitendo hivi ni dhambi. Hata hivyo wengine wanajisikia kwamba kutenda hivyo kwao ni dhambi.Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi. … Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza(m.14, 20). Hiyo ni kutokana na udhaifu wao wa imani (m.2:Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga). Hapo ni muhimu kwamba kila mmoja afuate dhamiri yake, maana ni Mungu atakayetuhukumu wala si mwanadamu.Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu(m.10-12). Kama unaweza kwa moyo mweupe kumshukuru Mungu kwa kile unachokitenda, basi, usiwe na wasiwasi.Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu (m.5-6). Kol 3:17 uwe mwongozo wetu:kila mfanyalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye!

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/