Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 8 YA 29

Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lo lote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa(m.21). Mafundisho haya hutusaidia k.m. Wakristo wakiwa na maoni tofauti juu ya matumizi ya divai (mvinyo) na pombe. Mtu akinywa sana hulewa, na ulevi ni dhambi katika Biblia.Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya(Lk 21:34; unaweza pia kusoma Gal 5:19-20 na Efe 5:18). Lakini kunywa kidogo tu kwa sababu ya kupenda ladha yake siyo dhambi:Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake(m.14).Kwa kuwa kila kiumbe cha Mungu ni kizuri, wala hakuna cha kutakaliwa, kama kikipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimetakaswa kwa neno la Mungu na kwa kuomba(1 Tim 4:4-5; unaweza pia kusoma Yn 2:9-10). Siyo dhambi - isipokuwa ikiwa ni pombe ya tambiko (1 Kor 10:19-21,Basi niseme nini? Ya kwamba kile kilichotolewa sadaka kwa sanamu ni kitu? Au ya kwamba sanamu ni kitu?Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo sadaka wavitoa kwa mashetani, wala si kwa Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani. Hamwezi kunywea kikombe cha Bwana na kikombe cha mashetani.Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani). Ila hata ukiweza kunywa kidogo kwa moyo mweupe mbele ya Mungu, itakuwa nidhambikufanya hiviikiwaitamkwaza nduguyo.Basi tusizidi kuhukumiana, bali afadhali toeni hukumu hii, mtu asitie kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha. …Na ndugu yako akiingia huzuni kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. (m.13 na 15; rudia pia m.19-22).

siku 7siku 9

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/