Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe(m.1). Nguvu katika imani ionekane kwa namna wenye imani wanavyoshirikiana na walio dhaifu katika imani. Waache vitendo vinavyowakwaza. Wasilete ugomvi kwa mambo yasiyo na msingi kwa imani.Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe(m.2). Nayeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, walakini msimhukumu mawazo yake(14:1). Bali wote wanie mamoja (m.5),maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu ... tufuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana(14:17, 19).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/