Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Neno la Kigriki lililotafsiriwamhudumu wa kanisanidiakonon,yaani mdiakonia (m.1; huhusu wajibu huu katika kanisa unaweza kusoma Mdo 6:1-6 na 1 Tim 3:8-11 ambapo nenodiakononpia imetumika). Nafasi hii hushikwa pia na wanawake.Fibini mwanamke. Paulo alimjua, maana Kenkrea uko jirani na Korintho alipokuwepo Paulo akiandika barua hii kwa Warumi. Neno lililotafsiriwamsaidizi(m.2) ina maana ya mtu aliyepokea na kuwasaidia wageni. Sasa mwenyewe hutumwa Rumi kama mgeni akiichukua barua ya Paulo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/