Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Ni muhimu kukumbuka matendo makuu ya Mungu kwetu. Hili ndilo kusudi la matukio mawili katika somo: kuweka wakfu mzaliwa wa kwanza, na sikukuu ya mikate isiyotiwa chachu. Wakati tukio la kwanza linatukumbusha Mungu alivyomkomboa mzaliwa wa kwanza kwa damu ya mwanakondoo, tukio la pili huashiria maandalizi ya kuondoka utumwani. Mungu ametukomboa sisi pia kutoka katika utumwa wa dhambi. Alimtuma Yesu aliye mzaliwa wa kwanza afe msalabani kwa ajili ya dhambi zetu. Msalaba ni alama ya ukombozi wetu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/