Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 15 YA 29

Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana(m.22). Huyu Tertio alikuwa karani wake Paulo wakati wa kuandika barua hii. Mara mbili Paulo hurudia maneno haya:Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi(m.20, 24).Ni neema hiyo ambayo ameielezea kwa bidii na ujuzi katika barua hii. Ni neema kubwa ajabu! Kwa hiyo anamalizia barua kwa kumtukuza Mungu aliyetufunulia neema yake hiyo:Atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele,ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani.Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina(m.25-27)! Tafadhali, ndugu msomaji, amini neema iliyofunuliwa katika Yesu Kristo (m.26)!

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/