Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Farao alipoambiwa kwamba Waisraeli wameoondoka akabadili mawazo (m.5:Mfalme wa Misri aliambiwa ya kuwa wale watu wamekwisha kimbia; na moyo wa Farao, na mioyo ya watumishi wake, iligeuzwa iwe kinyume cha hao watu, nao wakasema, Ni nini jambo hili tulilotenda, kwa kuwaacha Waisraeli waende zao wasitutumikie tena?). Yeye na watu wake wakaamua kuwafuata Waisraeli ili kuwarudisha utumwani Misri. Ni kitu gani kilichombadili mawazo? Kwa nini anataka kupinga mapenzi ya Mungu? Jibu ni Mungu mwenyewe! Ubinafsi ulimtawala Farao kiasi cha kutokubali kupoteza nguvukazi. Kumbe kusudi la Mungu kuwatoa Waisraeli utumwani ni ili wawe huru na kumtumikia. Mungu mwenyewe anamwambia Farao habari hiyo:Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia(4:23). Hakuna wa kupinga kusudi hili. Mungu ametupa nafasi ya kumtumikia kwa hiari na uaminifu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/