Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 10 YA 29

Mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe(m.7). Tofauti za Wakristo kuhusu kula na kunywa ziliwazuia kutembeleana kwa uhuru. Pakawepo kama makundi mawili. Lakini mambo kama haya yasiwatenganishe! Bali wapeane heshima. Waufuate mfano wa Kristo! Yeye hakujipendelea mwenyewe (m.3:Kristo … hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi). Aliwakaribisha wote. Ni Mwokozi wa wote. Ni Mwokozi wa Wayahudi kutokana ahadi kwa babu zao, na Mwokozi wa Mataifa kutokana na rehema zake.Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu;tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa, Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa, Nami nitaliimbia jina lako(m.8-9)!

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/