Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Paulo ameandika 14:1-15:13 kwa ujasiri ili kuwakumbusha. Hata hivyo anaamini kwamba wao wenyewe wanaweza kuonyana, maana wamekomaa katika imani (m.14-15:Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana. Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu). Paulo alijitoa sana kwa huduma ya Injili ili atimize wajibu aliopewa na Mungu ya kuwa Mtume wa Yesu Kristokwa Mataifa(unaweza kusoma zaidi kwa kulinganisha m.16-19 na Mdo 9:15 na 20:24). Alijitahidi sana kuhubiri Injili sehemu zote za ulimwengu uliojulikana kwa wakati ule, yaani Utawala wa Warumi (m.19b-21). "Iliriko" (m.19) ni eneo la bara Ulaya. Lengo sasa ni Spania (m.28).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/