Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Sehemu hii ya mafundisho ya Paulo (14:1-15:13) inahusu kwamba Wakristo wanatofautiana kwa namna wanavyoishi maisha yao ya kila siku, ingawa wana shabaha hii moja kwa maisha yao. Tatizo analoona kwao si imani yao. Wawe na imani dhaifu au imani yenye nguvu, umuhimu ni kwamba wanafanya yote kwa Bwana. Wenye imani wote ni wa kanisa la Bwana,kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana(m.6-8). Bali tatizo lao (dhambi yao) ni kwamba wenye nguvu wanawadharau walio dhaifu, na walio dhaifu wana mashaka juu ya wenye nguvu na kuwahukumu. Kwa hiyo Paulo anasisitiza kwambayeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali(m.3)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/