Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Paulo anamaliza kufafanua maana ya kutoa miili yetu katika kumtumikia Mungu (12:1,Kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana). Anatoa tena mkazo juu ya upendo (m.8-10). Halafu anasisitiza kuwa kurudi kwa Bwana Yesu ni karibu (m.11-14). Kwa hiyotuyavue matendo ya giza, na ... mvaeni Bwana Yesu Kristo(m.12, 14).Kwa imani tumekwisha vua matendo ya giza na kumvaa Bwana Yesu.Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo(Gal 3:26-27). Basi, imani hiyo ionekane katika matendo! Mwuguzi huvaa nguo za kiuguzi! Vilevile Mkristo avae nguo za Kikristo, yaani awe na mwenendo wa Kikristo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/