Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 4 YA 29

Naona Wakristo wa Tanzania wameyazingatia sana mafundisho haya, maana Tanzania ni nchi pekee Afrika ambayo haijawa na vita vya ndani kwa ndani. Huwaheshimu wanaostahili heshima tukiamini mamlaka ya nchi hayapatikani bila kibali cha Mungu (m.1-2:Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na ile iliyopo imeamriwa na Mungu. Hivyo amwasiye mwenye mamlaka hushindana na agizo la Mungu). Kwa hiyowapeni wote haki zao, mtu wa kodi, kode; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima(m.7). Ni halali kuwa na maoni na siasa tofauti na serikali iliyopo, lakini si halali kuivunja sheria ya nchi ili kuyafanya maoni yako yashinde. Lazima utumie njia zinazokubalika ukitaka kuendeleza siasa yako! Pia tuwaombee viongozi wa nchi:Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli(1 Tim 2:1-4)!

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/