Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

SIKU 3 YA 29

Leo Mtume Paulo anaagiza juu ya ule wajibu ambao ni sawa kwa Wakristo wote! Neno kuu ni upendo! Upendo unatuunganisha kama damu inavyoviunganisha viungo mwilini. Paulo anatuagiza tufanye matendo ya upendo yasiyo kawaida katika ulimwengu huu:Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani(m.14).Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote(m.17).Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema(m.21)! Huenda unasema: "Yatawezekana kweli haya? Naona mimi siwezi!" Lakini ndivyo Bwana wako anavyotaka uishi na kukuwezesha kwa upendo wake mwenyewe.Kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi(Rum 5:5).Sisi twapenda kwa maana yeye[Mungu]alitupenda sisi kwanza(1 Joh 4:19).Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi(Yn 13:34-35). Kupendana kwetu kutawafanya wengine wavutwe kwa Yesu!

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023

Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/