Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023Mfano
Katika m.1-2 Paulo amesema juu ya kujitoa kwetu kwa Bwana na kuhusu kujua mapenzi yake katika maisha yetu. Ndipo kuanzia 12:3 hadi 13:14 anafafanua mambo haya zaidi. Leo ni juu ya wajibu wa Wakristo. Hutofautiana kutokana na zile karama za Roho walizopewa kwa neema. Kuna shughuli za aina mbalimbali zinazohitaji kufanyika katika kanisa. Ni muhimu kiongozi asichukue mzigo mkubwa kuliko atakavyo Mungu, bali agawanye majukumu! Tutegemeane kama viungo mwilini mwetu.Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja;vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake(m.4-5; ukitaka kujifunza zaidi juu ya jambo hili, soma Mdo 6:1-7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku /Novemba 2023 ni mpango mzuri wa kusoma biblia kila siku sehemu kwa sehemu kwa mwezi wa Novemba pamoja na maelezo mafupi ya kukusaidia kutafakari somo ulilosoma. Katika mpango huu utasoma zaidi kitabu cha Kutoka na Warumi. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: https://www.somabiblia.or.tz/