Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Kama alivyoanza katika m.13, Daudi anahitimisha zaburi hii kwa maneno ya sifa. Jambo kuu ni kumshukuru Mungu kwa jinsi alivyompigania. Daudi alimtegemea Mungu kama mwamba na wokovu wake (m.46, Ahimidiwe mwamba wangu; na atukuzwe Mungu wa wokovu wangu). Kwa hiyo alijikabidhi kwake katika hali zote. Hata sasa baada ya kuinuliwa juu sana, Daudi anaendelea kumtegemea Mungu. Katika m.50b anasema, Amfanyia fadhili masihi wake, Daudi na mzao wake hata milele. Hapo anaonyesha imani yake katika ahadi ya Mungu kwa Daudi, kama tunavyoisoma katika 2 Sam 7:16: Na nyumba yako, na ufalme wako, vitathibitishwa milele mbele yako. Nacho kiti chako kitafanywa imara milele. Angalia kuwa kwa njia hiyo habari ya wokovu wa Mungu iliwafikia hata watu wa mataifa (m.49, BWANA, nitakushukuru kati ya mataifa), na mfalme Daudi alipata kuwa mfano wa Masihi, yaani, Kristo Yesu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz