Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Injili ya Luka mara kwa mara inaeleza kwamba Yesu alitafuta nafasi ya kuomba. Sasa mfano wake umewapa wanafunzi wake hamu ya kujifunza kuomba. Kwa mazingira ya wakati ule ilikuwa ni jambo la kawaida mwalimu wa dini kuwafundisha wanafunzi wake sala maalumu ya kuomba. Na kawaida ni kwamba sala ya aina hii iombwe mara tatu kwa siku, yaani asubuhi, mchana na usiku. Injili ya Mathayo imeandika kwa kirefu ‘Sala ya Bwana’ hivi: Baba yetu uliye mbinguni, Jina lako litukuzwe, Ufalme wako uje, Mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina (Mt 6:9-13). Mara tatu kwa siku Yesu anataka umwite Baba na kumwomba mambo haya k.m. msamaha wa dhambi!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz