Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 4 YA 31

Kizazi hiki ni kizazi kibaya; kinatafuta ishara (m.29). Wayahudi walikuwa na mioyo migumu sana. Walibarikiwa kipekee sana. Mwana wa Mungu yu katikati yao na kufanya miujiza mingi. Hata hivyo wengi hawataki kuamini. Bado wanataka ishara zaidi. Lakini kutaka hivyo ni kumjaribu, kama ilivyoandikwa katika m.16, Walimjaribu, wakimtaka ishara itokayo mbinguni. Ndiyo maana Yesu akawaambia, Ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia (m.20). Ukweli ni kwamba wao wametawaliwa na Shetani wala siye Yesu. Kwa maana Yesu anasema, Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu asiyekusanya pamoja nami hutawanya (m.23). Je, wewe kweli u pamoja naye?

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz