Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Kwa kuwa hazina yenu ilipo, ndipo itakapokuwapo na mioyo yenu (m.34). Yesu anazidi kutufundisha juu ya hatari ya choyo akisema, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo (m.15). Anataka Mungu awe wa kwanza katika maisha yetu, maana maisha yetu ya sasa ni mafupi sana tukilinganisha na maisha ya baadaye ambayo ni ya milele. Na kama Mungu hajaupata moyo wako katika maisha haya utakuwa bila Mungu milele na milele baada ya kufa. Utakuwa katika mateso ya Jehanum. Maana Mungu ana uweza wa kumtupa [mtu] katika Jehanum (12:5). Lakini kumbuka pia Yesu anavyosema katika m.32, Msiogope, enyi kundi dogo; kwa kuwa Baba yenu ameona vema kuwapa ule ufalme. Tena, kuwa mtoto wa Mungu ni baraka sana pia kwa maisha haya ya sasa, maana hututunza sana. Ni Baba mwaminifu ambaye huwatunza watu wake zaidi ya anavyotunza majani ya kondeni! Kwahiyo utafuteni ufalme wa Mungu, na hayo mtaongezewa (m.28-31).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz