Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano
Leo wito mkubwa wa Yesu kwa wafuasi wake ni kwamba tuwe waminifu kila mmoja wetu mahali pale Bwana alipotuita kulitumikia kanisa lake. Kila Mkristo ana wajibu wake. Wote tunadaiwa kupendana, kuwaleta wengine kwa Yesu, kuutafuta uso wa Bwana katika maombi, kulisikiliza Neno la Mungu kanisani na kushiriki katika Chakula cha Bwana. Tusipodumu katika hayo pamoja na huduma zingine tunazoitiwa kanisani, basi hatutakuwa tayari Bwana akija! Heri watumwa wale, ambao bwana wao ajapo atawakuta wanakesha (m.37).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure
More
https://www.somabiblia.or.tz