Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

SIKU 10 YA 31

“Ubatizo” (m.50), maana yake hapa ni kile kipindi kigumu cha mateso na kufa kilicho mbele ya Yesu kama alivyowauliza wanafunzi, Mwaweza kunywea kikombe ninyweacho mimi, au kubatizwa ubatizo nibatizwao mimi? (Mk 10:38). Katika m.56-57 Yesu anauliza, Imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya? Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Wanayotakiwa kutambua na uamuzi wa haki wanaotakiwa kufanya ni kwamba sasa kweli kwa njia ya Yesu Ufalme wa Mungu umekaribia kwao. Ndiye Kristo, Mwana wa Mungu. Ni wito mkubwa wa Mungu kwa Waisraeli! Watubu na kumwamini! Na ni hatari kubwa mno kutojali. Ndivyo Yesu anavyosisitiza, akitoa mfano huu, Unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidii kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani; Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho (m.58-59)!

siku 9siku 11

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022

Soma Biblia Kila Siku Disemba/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Disemba pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa siku husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Luka na Zaburi. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure

More

https://www.somabiblia.or.tz